Msichana wa miaka kumi na moja anauguza majeraha baada ya mamake kumpiga kwa kigezo cha kumwadhibu .


  Inadaiwa kuwa mama huyo ana mazoea ya kumpiga mtoto huyo , ishara kamili ikidhihirishwa na alama ambazo msichana huyo yuko nazo mwilini. Aidha majirani wanadai kuwa mtoto huyo hufungiwa nyumbani pekee yake na hata amelazimika kuwacha shule. Majirani waliripoti kesi hiyo na kwa sasa polisi wanatarajiwa kuanzisha uchunguzi. Watch KTN Live http://www.ktnkenya.tv/live Follow us on http://www.twitter.com/ktnkenya Like us on http://www.facebook.com/ktnkenyav <iframe width=”560″ height=”315″ src=”//www.youtube.com/embed/F5hGOujGBNg” frameborder=”0″ allowfullscreen>

HAYA NDIO MAPYA KUHUSU NDEGE YA MALAYSIA ILIYOTOWEKA ANGANI


Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia amesema Shirika Kuu la Kijasusi la Marekani CIA linaficha maelezo muhimu kuhusu hatima ya ndege ya Malaysia iliyotoweka. Katika taarifa aliyochapisha katika weblogu yake siku ya Jumapili, Mahathir Mohammad amesema CIA na shirika la utengenezaji ndege la Marekani, Boeing, kwa pamoja zinaficha maelezo kuhusu ndege iliyotoweka. Aidha amesema ni…

CHADEMA yatangaza Baraza Kivuli la Mawaziri Jipya 2014 likihusisha vyama vingine!


hatimaye Baraza Kivuli la Kambi ya Upinzani Bungeni liko hewani kama ifuatavyo; WAZIRI MKUU KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI (KUB) MIZENGO KAYANZA PETER PINDA FREEMAN AIKAELI MBOWE WIZARA WAZIRI WA CCM NAIBU WAZIRI CCM WAZIRI KIVULI NAIBU WAZIRI KIVULI (UKAWA) (UKAWA) 1 OFISI YA RAIS CAPT. GEORGE PROF. KULIKOYELA (UTAWALA BORA) MKUCHIKA KAHIGI(CHADEMA) 2 OFISI YA…

HII NDIO BAJETI YA 2014/15 :


Bunge la bajeti linaanza kesho huku Serikali ikiwa imetoa mwelekeo wa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2014/15 kuwa ni Sh19.6 trilioni, ikilinganishwa na Sh18.2 za Bajeti iliyopita. Vipaumbele vya bajeti hiyo ni kuendeleza Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ulioanza mwaka 2011 na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ambao unajumuisha maeneo sita ya…

Sudan Kusini:Mauaji ya kikabila Bentiu


Waasi nchini Sudan Kusini Umoja wa Mataifa unasema kuwa vikosi vinavyoipinga serikali nchini Sudan Kusini viliwaua mamia ya watu kwa sababu ya kabila lao wakati vilipouteka mji wa Bentiu wiki jana. Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo, watu hao walilengwa wakiwa katika maeneo salama walikokuwa wanahifadhiwa kama vile msikitini, makanisani na hospitalini. Umoja huo…

Mbunge auawa na Al Shabaab Mogadishu


Gari ambalo lilikuwa na bomu lililokuwa limetegwa na Al Shabaab Mbunge mmoja ameuawa katika shambulizi la bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari mjini Mogadishu Somalia. Kundi la wanagmabo la Al Shabaab limekiri kufanya shambulizi hilo dhidi ya mbunge Isak Mohamed Rino. Mbunge mwingine Mohamed Ali, alijeruhiwa katika shambulizi hilo ambalo limetokea huku serikali ikiwa mwenyeji…

Nigeria:Wazazi wawasaka watoto msituni


Shule ya mabweni iliyovamiwa huku wasichana zaidi ya miamoja wakitekwa nyara Wazazi wa takriban watoto miamoja waliotekwa nyara na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Boko Haram wameingia msituni kuwatafuta watoto wao. Wasichana hao walitekwa nyara kutoka shuleni mwao katika eneo moja la vijijini Kaskazini Mashariki mwa Nigeria Jumatatu usiku. Mwandishi wa BBC nchini…

Mafuriko Dar: Watu 25 wathibitika kufa


Mafuriko Dar es Salaam, Tanzania Watu 25 wamethibitika kufa mkoani Dar es Salaam nchini Tanzania kutokana na mvua kubwa zilizonyesha kwa siku tatu mfululizo kuanzia Ijumaa hadi Jumapili iliyopita. Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Sadik Meck Sadik amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo akisema watu wengine 14 wanadaiwa kufa, lakini hawajathibitishwa…

FERRY MOJA YAZAMA KOREA


Ferry yenye abiria 460 ikizama Korea Kusini. Oparesheni ya uokozi inaendelea kufuatia ishara za dharura zilizoripotiwa kutoka meli moja ilioyobeba takriban abiria 460 katika pwani ya Korea Kusini. Maafisa wanasema kuwa walinzi wa pwani hiyo, meli za wanamaji wa Korea pamoja na ndege za uokoaji , zimepelekwa katika ferry moja inayozama kusini mwa pwani hiyo….

BREAKING NEWS: KUHUSU TAARIFA ZA KIFO CHA MWANAMUZIKI MZEE GURUMO.


Kuhusu mwanamuziki mkongwe mzee Gurumo kufariki dunia. mzee wa siku nyingi sana kwenye muziki Tanzania ambae aliwahi kuingia kwenye vichwa vya habari mara nyingi hasa kutokana na kuugua kwake kuliko mfanya aache hata muziki aliokua anaufanya. Taarifa zilizothibitishwa na hospitali ya Taifa Muhimbili kwa zimesema Mzee huyu amefariki dunia akiwa hospitalini hapo leo April 13…

PISTORIUS AANDAMWA NA MUONGOZO MASHTAKA WA KESI YAKE


Mwanariadha wa Afrika kusini Oscar Pistorius amerejea tena mahakamani kuhojiwa zaidi na kujibu maswali ya mwendesha mashtaka mkuu Gerrie Nel katika kesi anayoshtumiwa kwa kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake mwanamitindo Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwezi februari tarehe 14 mwaka uliopita . Bwana Nel amekuwa akimwandama Pistorius , akisema hakuwa mkweli katika toba yake na…