Clouds Media yapata leseni ya urushaji wa matangazo katika nchi za falme za kiarabu


Kampuni ya Clouds Media International leo imetangaza
kuwa imepewa leseni ya kurusha matangazo katika nchi
za umoja wa falme za kiarabu (UAE). Akielezea kuhusu
leseni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo
Bwana Joseph Kusaga, amesema sasa kituo cha Clouds
TV kimataifa kitakuwa kikishuhudiwa na watu wa
mataifa mbalimbali.

image

Joseph Kusaga
Clouds TV kimataifa ni mwendelezo wa televisheni
maarufu sana kwa vijana nchini Tanzania, hata hivyo
sehemu kubwa ya maudhui yatakayokuwemo kwenye
Clouds TV kimataifa itakuwa na mpangilio mpana wa
vipindi kwa watazamaji vitakavyorushwa kwa lugha za
Kiingereza na Kifaransa.
Akieleza zaidi Kusaga amesema, “Leo ni siku ya
kihistoria na alama ya hatua moja katika mpango wetu
wa kina wa kupeleka maudhui ya Clouds TV kimataifa
kupitia matangazo kwa njia ya mitandao.”
Clouds TV kimataifa haitotoa tu burudani, lakini pia
itakuwa kiunganishi kwa waafrika waishio katika umoja
wa nchi za falme za kiarabu pamoja na kuwapa fursa za
kutangaza bidhaa zao na kuimarisha uhusiano baina
yao. Vituo vya televisheni katika Umoja wa falme za
kiarabu vipo vingi na vyenye ushindani mkubwa, lakini
Clouds TV kimataifa imebahatika kupata nafasi ya
kurusha matangazo yatakayowafikia walengwa katika
chaneli yenye uwezo wa kuwahudumia zaidi ya
watazamaji takribani milioni 3.5 kutoka katika nchi za
Afrika. Kwa sasa hakuna kituo kinachotoa huduma hii
na hivyo kuwa fursa muhimu kwa watazamaji.
Clouds TV kimataifa itarusha vipindi vya burudani,
tamthilia, maigizo, ucheshi, na muziki, vyote vitakavyo
kuwa vimeandaliwa kutoka nchi za Mashariki,
Magharibi na Kusini mwa bara la Afrika na itapatikana
kwa watazamaji walio katika Umoja wa falme za
kiarabu kupitia huduma ya IPTV inayotolewa na Etisalat
na Du.
Clouds TV kimataifa itarushwa kupitia mamlaka ya Abu
Dhabi ijulikanayo kama twofour54, ikiungana na vituo
kama FOX na CNN. Clouds TV kimataifa itaanza
kurusha matangazo ya majaribio katika wiki chache
zijazo kabla ya tarehe 15 mwezi June mwaka huu.

China kutengeneza ‘lifti’ yenye kasi zaidi duniani inayoweza kupanda ghorofa 95 kwa sekunde 45


Kampuni ya Hitachi imetangaza
mpango wake wa kutengeneza lifti
yenye kasi zaidi duniani (The world’s
fastest ultra-high-speed elevator)
katika jengo refu la Guangzhou CTF
Finance Centre linalojengwa huko
Guangzhou, China.

image

Mchoro wa jengo hilo refu la
Guangzhou CTF
Jengo hilo linalotazamiwa
kukamilika ifikapo mwaka 2016,
litakuwa na lift hizo zenye uwezo wa
kwenda kasi ya kupanda au kushuka
ghorofa 95 kwa sekunde 45.
Hitachi wamesema lifti hizo
zitatumia teknolojia ambayo
inahakikisha usalama kwa watumiaji,
hivyo wasafiri watakuwa wakisafiri
salama na kwa raha pamoja na
mwendo wake mkali.

image

Ujenzi wa kikwangua anga hicho cha
CTF ulianza mwaka 2010 na picha
hii ilipigwa 23 December 2012, na
linatarajiwa kukamilika mwaka 2016.
Source: Daily Mail & BONGO5

AFISA MKUU WA FACEBOOK ‘SHERYL SANDBERG’ AWAHIMIZA WANAWAKE KUSHIKILIA NAFASI MUHIMU KATIKA BIASHARA


image

Muanzilishi wa mtandao wa
Facebook Mark Zuckerberg akiwa
ameketi na Sheryl Sandberg
Afisa mkuu wa mipango wa
Facebook,
mwanamama Sheryl
Sandberg amewahimiza wanawake
wenzake Duniani kote kuacha
kubweteka na kuwa tegemezi bali
kutakiwa kushikilia nafasi muhimu
katika biashara.
”Ukiwa unatafakari kufanya kitu,
jiulize nini unachoweza kufanya,
ikiwa hauna uwoga na basi ukifanye”
alisema Sandberg wakati
alipofanyiwa mahojiano na kituo cha
utangazaji cha BBC.
Sherly Sandberg ni mwanamke wa
kwanza kushikilia wadhifa huo
katika kampuni ya Facebook tangu
mwaka 2012, huku mwaka jana
akiwa ameandika kitabu ‘Lean In’ na
katika kitabu hicho anawashauri
wanawake waanze kushikilia vyeo
katika meza za maamuzi.
Alikuwa anawaambia ni jinsi gani
wanavyoweza kupiga hatua za nafasi
zao za kazi na kusema kuwa ni
muhimu sana kwa wanawake ambao
nusu ya idadi ya watu wote waanze
kushikilia vyeo katika meza za
maamuzi, lakini bado alisema
hatujafika hapo.
Alisema Wanawake wanaweza kuwa
viongozi muhimu sana katika
biashara, Serikali na pamoja na
kuwa wajasiriamali.
”Dunia inashuhudia mageuzi
makubwa ya kiteknolojia ambayo
yanahusisha simu ya rununu na
facebook ipo katikati ya mageuzi
hayo” alisema Sandberg alipokuwa
akizungumzia changamoto
zinazoikumba mtandao wa Facebook

RAIS BARACK OBAMA AMKARIBISHA MAKAMU WAKE KWENYE ULIMWENGU WA SELFIE NA INSTAGRAM


Katika kuonyesha kunogewa na
mtindo mpya wa picha ‘SELFIE’. Rais
wa marekani Barack Obama
amemkaribisha makamu wake wa
Rais ‘Joe Biden kwenye mtandao wa
Instagram kwa staili ya kupiga picha
‘Selfie’ pamoja iliyowekwa kwenye
akaunti rasmi ya kiongozi huyo
ambayo ina wafuasi wapatao Laki 1
na ushee.

image

Rais Barack Obama na Makamu
wake wa Rais Joe Biden
wakitokelezea katika SELFIE.
”Found a friend to join my first selfie
on Instagram. Thanks for following
and stay tuned. –VP” aliandika Biden
kwenye ukurasa wake wa Instagram,
wakati Obama aliandika ”Welcome
to Instagram, Mr. Vice President.”
kupitia ukurasa wake wa Facebook.
Unaweza ukatazama picha nyingine
zaidi za makamu huyo wa Rais
alizokwisha kuziweka kwenye
ukurasa wake tangu ajiunge rasmi na
Insta Aprili 16 mwaka huu, akiwa
tayari ameshapakia picha tano ndani
ya kipindi cha siku 3 tu. Chezea insta
wewe

HIVI NDIVYO MUONEKANO MPYA WA TWITTER UTAKAVYOKUWA


Ukurasa wako wa Twitter upo mbioni
kuwa na muonekano mpya. Twitter
imetangaza jana kuwa itazindua
muonekano mpya na vitu vipya
kwenye kurasa za watumiaji.

image

Kampuni hiyo imesema mabadiliko
hayo yatafanya vitendo vya kujieleza
binafsi kwenye mtandao huo wa
kijamii kuwa rahisi na kwa raha
zaidi. Muundo mpya wa Twitter
unawapa watumiaji picha kubwa
zaidi ya profile pamoja na picha ya
juu yake maarufu kama header
image.
Twitter imesema profile mpya
itamulika tweets maalum na
kuwaruhusu watu kutafuta kwenye
kurasa zao kupata tweets
wanazozitaka. Kwa mfano, followers
wanaweza kuchagua kuona tweets
zenye picha na video ama majibu
kwenye mjadala Twitter. Pia tweets
zenye retweets na majibu mengi
zitaonekana kwa ukubwa zaidi ili iwe
rahisi kwa watu kuziona.
Muundo huo mpya kwa sasa upo
kwa watumiaji wachache na
wamesema utatokea kwa wote wiki
chache zijazo. Miongoni mwa
watumiaji wa Twitter wenye muundo
huo mpya ni pamoja Michelle Obama
(@flotus), bondia Floyd Mayweather
(@FloydMayweather), na muigizaji
Kerry Washington (@
kerrywashington).
CREDIT: By CNN