Category Archives: KICHUPA

KUCHUPA: “PHD On my Wedding Day Official Video Full HD” on YouTube


image

image

Baada ya Rest of my Life kufanya vizuri kwenye
vituo mbalimbali vya redio nchini, Muigizaji na
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hemedy
Suleiman ‘PHD’ au unaweza ukamwita
PappiNation amekuja na ujio mwingine wa video
mpya ya wimbo wake ‘On My Wedding Day’
ikiwa ni miezi michache kupita tangu mkali huyo
amuanike mkewe mtarajiwa. Video
imetengenezwa na Kwetu Studio chini ya
muongozaji wake Msafiri Shabani.. Itupie Jicho
Hapo Chini…

image

PappiNation akiwa na kifaa chake AKA Mke
Mtarajiwa

PIGA KOPE KTK KIDEO CHA “MB DOG — MBONA UMENUNA (OFFICAL VIDEO)” on YouTube


Ukamilifu wa video hii ambayo picha zake
niliziweka hapa wiki chache zilizopita ni huu
hapa japo video hii ilikamilika wiki kadhaa
nyuma lakini walikua wakisubiri muda sahihi
wa kuitoa, ukisha itazama usiache kuandika
comment yako alafu baadae MB Dogg atapita
kusoma watu wake wamemuandikia nini.
Bonyeza play kutazama.

Video Mpya Ya Trey Songz – Smart Phones [Official Video]” on YouTube


Trey Songz ametoa video ya wimbo
wake mpya “SmartPhones” inayotoa
piha halisi ya kijana anayeishi
maisha ya starehe,burudani na ngono
nyingi mpaka kupelekea kupoteza
mpenzi wake na mahusiano yake
kuharibika. Trey katikati ya video
anabadilisha mawazo na kurudi
nyumbani kuokoa mahusino yake.
Trey Songz – SmartPhones [Official Video]: http://youtu.be/7sExF5B4G-U

image

VIDEO : KANYE WEST AMPA SHAVU LA KUMSIKILIZA SHABIKI ALIYEDAI ANAUWEZO WA KUCHANA ZAIDI YAKE


image

Kanye akimsikiliza shabiki aliyekuwa akiimba mbele
yake.
Rapa na Mmiliki wa lebo ya GOOD Music ‘Kanye West’
mwishoni mwa wiki aliamua kumpatia nafasi ya
kumsikiliza shabiki mmoja aliyeonekana kuwa msanii
asiye na jina wa miondoko ya kufokofoka, wakati
alipokuwa akirudi kwenye makazi yake aliyokuwa
amepanga ya Soho eneo la west Hoolwood, mjini Los
Angels, Marekani,
Akiwa ameongozana sambamba na mpenzi wake Kim
Kardashian, kijana mmoja aliwafuata kwa nyuma na
kudai kuwa yeye ni mkali na angependa adhihirishe
uwezo aliokuwa nao mbele ya rapa huyo na baada ya
kupewa nafasi, msanii huyo aliweza kuimba kwa
mtindo wa freestyle hali iliyomvutia kanye na kumfanya
asimame pembezoni mwa nyumba yake huku
akimsikiliza na baada ya jamaa huyo kumaliza, Kanye
alimwambia amefanya vizuri lakini kwa wakati huo
anahitaji kwenda kupumzika.
Mpaka hivi sasa bado haijaweza kufahamika hatma ya
shabiki huyo kama ataweza kulamba shavu la
kusainiwa kwenye lebo ya rapa huyo licha ya uwezo wa
hali ya juu aliounyesha pasipo kujali uwepo wa kamera
nyingi zilizokuwa zikimmulika kipindi anachana mbele
ya hitmaker huyo wa Bounce.
Unaweza ukatazama hapo chini Tukio zima lilivyokuwa,
sio mchezo kumfata mtu kama Kanye West ambaye ni
miongoni mwa marapa wa kubwa na wenye mkwanja
mrefu, lakini huyu jamaa aliweza ingawa hii sio mara
ya kwanza kwani hata mwanamuziki Big sean aliweza
kupata shavu la kujiunga na Good Music kwa staili
inayofana na hii

KAnye  West Lets Fan Rap For Him In SoHo! HD HQ: http://youtu.be/RZajcsSa0fs