MAREKANI YAIONYA RUSSIA KUHUSU UKRAINE


image

Marekani imeonyesha wasiwasi wake
kuhusu kile ilichokitaja kama
harakati za kundi fulani linalotaka
kujitenga ambalo limekuwa
likisaidiwa na Urusi kuchochea
ghasia mashariki mwa Ukrain.
Kufuatia kutekwanyara kwa vituo vya
polisi katika miji kadhaa ya
mashariki mwa Ukrain ,waziri wa
maswala ya kigeni nchini marekani
John Kerry amesema kuwa
mashambulizi hayo ya watu
waliojihami na silaha za Urusi
yalifanyika kwa mpangilio.
Katika mazungumzo yao ya simu na
waziri wa maswala ya kigeni nchini
Urusi Sergei Lavrov,Kerry ameitaka
Urusi kusitisha mashambulizi kama
hayo la sivyo ikabiliwe na vikwazo
zaidi.
Urusi imeonya kuwa utumiaji wowote
wa nguvu nchini Ukrain utahujumu
harakati za kidiplomasia kumaliza
mgogoro huo.